ZEPHANIA LIFE HERBAL CLINIC
  • Home
    • Home - Eng
  • About
  • Service
  • Contact
  • Kipanda Uso, Sababu, Dalili Na Matibabu Sahihi
  • Hatari Za Kiafya Za Uzito Mkubwa Na Tiba Yake
  • Dawa ya Asili ya Bawasiri
  • ujuh
  • Pumu (Asthima): Sababu, Dalili, na Tiba Asili Iliyothibitishwa Kisayansi
  • BAWESI: Natural Hemorrhoid Remedy for Internal & External Healing
Zephania Life Herbal Clinic

KLINIKI MAALUMU YA NGUVU ZA KIUME

MADHARA YA KITAMBI

Jinsi kitambi kinavyoathiri nguvu za kiume

Picture
Unajitazama katika kioo, lakini unachukizwa! Unachukizwa na mwili wako mwenyewe. Hauna la kufanya, unabaki kuhuzunika tu. Tumbo! Tumbo!
Licha ya kuwa tumbo kubwa linaweza kuufanya mwili kuwa na muonekano mbaya usiopendeza, kwa hakika madhara yake kiafya ni makubwa zaidi kuliko ubaya wa sura yenyewe.
 
Katika lugha yetu ya Kiswahili, mafuta ya tumboni hujulikana kama “kitambi.” Lakini pia kuna majina mengi ya utani yanayotumika mtaani kukiita hicho kitambi, baadhi ya majina ni kama vile  tumbo la mtungi, kishikio cha mapenzi, tairi la akiba, tumbo la bia, friji n.k. Kwa nini watu walipachika majina kama hayo?
 
Katika miongo michache ya nyuma hapa kwetu Tanzania, na hata katika baadhi ya nchi duniani; baadhi ya watu kutokana na ukosefu wa elimu walivitazama vitambi kama dalili ya ustawi mzuri wa maisha, na hasa ndiyo sababu ya kuvitengenezea majina ya ziada.
 
Katika miaka ya hivi karibuni, watu wengi sana sasa wametambua vizuri kuwa kitambi ni tatizo kubwa la kiafya. Utawaona wako katika kumbi za michezo ya mazoezi ya viungo (gym), wengine wakiwa katika utaratibu maalumu wa chakula (dieting); na wengine wakiwa katika programu za tiba ili kupunguza mafuta hayo mwilini, na ikiwezekana kuyaondoa yote kabisa, yaani kukifutilia mbali kabisa hicho kitambi. Hata hivyo, wapo baadhi ya watu bado "wanauchapa" usingizi. Hao bado wanafanya utani na mafuta!Ukweli wa mambo ulivyo, kitambi hakina utani! Ukileta utani katika mafuta hayo ya tumboni, basi muda si mrefu utagonga hodi katika chumba cha daktari ukiwa tayari na kisukari (TYPE 2), au ugonjwa wa moyo, au kupooza, au saratani, au shinikizo la damu la kupanda (High Blood Pressure), au matatizo ya kibofunyongo, au ugonjwa wa ini (cirrhosis) huku hali ya kuishiwa nguvu za kiume ikiwa ni jambo linalokwenda bega kwa bega na kitambi. Je, hapo utaendelea kufanya utani na kitambi? Bado utaita tumbo la bia? Au kadha wa kadhaa? Hakika utakiita ni tumbo la kifo!
 
Hayo siyo mafuta mazuri kabisa, wala siyo mafuta ya kuyatania wala kuyachekelea! Ukiyafungulia mlango tu na kuyaruhusu yaweke maskani yake tumboni mwako, ni sawa na kuruhusu nyoka kukaa chumbani mwako, hatima yake ni nini? Bila shaka ni kung’atwa! Kama zisipofanyika juhudi za haraka za kuidhibiti sumu ya nyoka huyo, basi matokeo yaweza kuwa kifo! Kitambi pia, ni vivyo hivyo.
 
Wakati mafuta mengi yanapokuwa mwilini huleta tatizo. Lakini mafuta haya ya tumboni yana hatari kubwa zaidi hata kama ni madogo.
 
Baadhi ya watu kwa kutojua madhara ya vitambi, huchukulia mambo kwa wepesi, husema, “Tumbo langu ni dogo tu, ni kama halipo vile!” Kwa mtazamo wao, ni kwamba wanaweza kunusurika na madhara ya kitambi.
 
Ni kweli kwamba, watu wanatofautiana ukubwa wa matumbo. Kuna ambao matumbo yao ni madogo, au ndio yanaanza. Kuna wengine ni makubwa kiasi, na wengine makubwa zaidi kiasi ambacho huwafanya kupata taabu sana katika kufanya kazi zao mbalimbali za kila siku.
 
Lakini, ukweli wa mambo ulivyo ni kwamba, mafuta ya tumboni yanaweza kukuletea maradhi hata kama hauna uzito mkubwa au hauna tumbo kubwa.
 
Kwa nini mafuta ya tumboni yalete maradhi? Yana uhusiano gani na maradhi? Kwa nini yapunguze nguvu za kiume? Haya ni baadhi ya maswali ambayo yanaweza kugonga katika akili ya msomaji.

Ukweli ni kwamba, tumbo kubwa ni matokeo ya mafuta mengi mno yaliyoweka makazi yake ndani kabisa ya tumbo au fumbatio (abdomen) na kitabibu yanajulikana kama “visceral fat.” Mafuta hayo huzonga na kudhuru figo zako, ini na viungo vingine vilivyo tumboni na kuharibu utendaji wa kazi wa viungo hivyo na kuvuruga utendaji wa homoni.
 
Ni mafuta ambayo huleta madhara makubwa katika mishipa yako ya damu. Seli za mafuta hayo huzalisha homoni na sumu ambazo moja kwa moja huathiri afya na tabia yako.
 
AINA YA MAFUTA YALIYO TUMBONI
Lakini, kabla hatujaenda kuangazia kwa undani uhusiano wa kitambi na magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa nguvu za kiume ambacho ndiyo kilio cha wanaume wengi wenye vitambi, kwanza ni muhimu tufafanue kwa ufupi aina za mafuta yaliyo tumboni.
 
Tumboni kuna mafuta ya aina mbili. Aina ya kwanza ni mafuta yanayotokea chini ya ngozi ya tumbo. Mafuta haya unaweza kuyagusa kwa nje kwa kufinya ngozi ya tumbo. Mafuta haya hayana madhara yoyote na yana msaada mkubwa kwa viungo vilivyo ndani ya tumbo, hukaa kama mto (cushion) kwa viungo kujiegemeza. Kitabibu mafuta haya huitwa, “Subcutaneous fat.”  
 
Aina ya pili ya mafuta, ni mafuta ambayo kitabibu huitwa, “Visceral fat,” ambayo nimekwisha yataja hapo awali. Haya ni mafuta ambayo hukaa ndani kabisa ya tumbo, hujitengenezea makazi yake karibu kabisa na ini na viungo vingine viliomo tumboni. Mafuta haya ndiyo tatizo na chanzo cha matatizo mengi ya kiafya katika mwili wako, na ndiyo mafuta tunayokwenda kujadili madhara yake katika makala haya, sababu ya kutokea kwake na ufumbuzi wake.
​
KISUKARI
Moja ya madhara ya kitambi ni kwamba, huweza kumfanya mtu apate ugonjwa wa kisukari kwa urahisi zaidi. Kwa sababu mafuta ya kitambi kwa ujumla huzonga viungo ambavyo husaidia kurekebisha sukari ndani ya damu.
 
Pindi insulini inapolielekeza ini kuhifadhi sukari ya akiba kwa ajili ya nishati ya baadaye, ini lililozongwa ndani tishu za mafuta hushindwa kuitikia ipasavyo. Matokeo yake, sukari huweza kuanza kujazana ndani ya mishipa ya damu na hivyo kuleta madhara makubwa katika viungo na kukaribisha ugonjwa wa kisukari.
 
Hali hiyo kitabibu huitwa “insulin resistance” ambapo seli za mwili hugoma kukubali homoni ya insulini. Insulini ni homoni ambayo hutolewa na seli za kongosho zijulikanazo kama beta cells. Hizi seli hutawanyika katika kongosho lote katika vishada vidogo vidogo vinavyojulikana kama visiwa (islets) vya Longerhans. Kazi kubwa za insulini huelekezwa kwenye umetaboli wa usimamizi wa kabohaidreti (sukari) na wanga, mafuta na protini.
 
Insulini pia hurekebisha kazi za seli za mwili, ikiwa ni pamoja na ukuaji. Insulini ni muhimu sana kwa matumizi ya mwili kama nguvu. “Insulin resistance” ni hali ambayo seli za mwili hugoma kukubaliana na insulini. Hii inaweza kuwa ni hali ya kawaida kama kiwango cha insulini kimepunguzwa. Matokeo yake viwango vikubwa vya insulini huhitajika ili insulini kufanya kazi yake vizuri. Hivyo, kongosho hufidia kwa kujaribu kutoa insulini zaidi. Mgomo huu hutokea katika mwili kuitikia insulini yake yenyewe (endogenous) au pindi insulini inapokuwa inaingizwa kwa sindano (exogenous).
 
Katika “insulin resistance” kongosho hutoa insulini zaidi na zaidi mpaka kufikia wakati sasa haliwezi tena kutoa insulini ya kutosha kwa ajili ya mahitaji ya mwili, hivyo sukari ndani ya damu hupanda.
Mshtuko wa moyo
​Kitambi kina urafiki mkubwa na ugonjwa wa moyo. Pindi unapokula chakula, kiwango chako cha insulini ndani ya damu hupanda. Kadiri sukari inavyopanda, ndivyo pia insulini nyingi inavyotolewa na kongosho ili kuendelea kuifanya sukari isipande juu zaidi.
 
Punde tu baada ya insulini kufanya kazi yake ya kushushua viwango vilivyopanda vya sukari, ini huondoa insulini kutoka ndani ya damu.
 
Hata hivyo, mafuta yaliyo ndani ya mikondo ya ini, huzuia na kukinza seli za ini kuondoa insulini kutoka katika mikondo ya damu.
 
Kwa hali hiyo, watu ambao hutunza mafuta mengi tumboni, wajue pia hutunza mafuta mengi katika ini zao, hali ambayo mafuta hayo huzuia ini kuondoa insulini ndani ya damu na hivyo kusababisha kuwa na kiwango kikubwa cha insulini.
 
Ni kwamba unahitaji insulini kuzuia viwango vya sukari ndani ya damu kupanda juu, lakini insulini nyingi hubana mishipa ya ateri na kusababisha mshtuko wa moyo.
 
Vyakula vya mafuta na ukosefu wa mazoezi husababisha ongezeko la uzito. Hali hii huzifanya njia katika mishipa ya damu kuwa miembamba zaidi na kukakamaa, matatizo ambayo hujulikana kitaalamu kama  atherosclerosis au arterioscloris. Huu ni mchakato wa kunenepa na kukamaa kwa kuta za ateri kubwa na ateri za ukubwa wa kati.  
 
“Arterioscloris” ni hali ambayo husababisha kutokea kwa maradhi ya ateri za moyo (coronary artery) ikipelekea kwenye ugonjwa wa moyo unaosababisha maumivu kifuani (angina) na mshtuko wa moyo, kupooza, na maradhi ya mishipa ya damu. Hii hutokana na lehemu (cholesterol) na baadhi ya vitu kujijenga katika kuta za mishipa ya damu.
 
Kama ujenzi huo wa lehemu utatokea katika mishipa mikubwa ya ateri karibu na moyo itasababisha mshtuko wa moyo, na kama itatokea katika mishipa midogo ya damu inayokwenda kwenye uume, kama tutakavyoeleza baadaye, itasababisha kushindwa kusimama kwa uume. Hali hii ya kushindwa kusimama kwa uume, kitabibu ni dalili ya tahadhari ya awali ya matatizo ya moyo.
 
Vipengele vinavyoweza kusababisha “arterioscloris” ni pamoja na “insulini resistance,” lehemu mbaya (LDL), shinikizo la damu la kupanda (HBP), uvutaji sigara, na kisukari.
 
Mshtuko wa moyo mara nyingi hutokea pindi damu inapoganda na hivyo kuziba mtiririko wa damu kupitia ateri ya moyo (coronary artery). Huu ni mshipa wa damu unaojaza damu inayokwenda sehemu za misuli ya moyo. Mtiririko wa damu ulioingiliwa unaweza kudhuru au kuharibu misuli ya moyo.
 
Mshtuko wa moyo pia huitwa myocardial infarction. Ni ugonjwa ambao mtu anaweza kujikuta katika hatari kubwa. Hii ni kwa sababu mara nyingi watu huchanganya dalili zake kwa kuziona ni za ugonjwa mdogo na hivyo kuchelewa kupata matibabu.
 
Watu wenye vitambi wako katika hatari kubwa ya kupata matatizo ya moyo kuliko watu ambao hawana vitambi.
Ni kwa namna gani kitambi huathiri nguvu za kiume
​Tumeona hapo juu kwa ucahe jinsi kitambi kinavyoathiri afya. Sasa tuangalie jinsi kitambi kinavyoathiri nguvu za kiume.

​MZUNGUKO WA DAMU
Kitambi kinaenda bega kwa bega na upungufu wa nguvu za kiume. Kwa nini? Kwa sababu kitambi huharibu mzunguko wa adamu. Tunahitaji mzunguko wa damu wenye afya kwa ajili ya damu hiyo kuingia ndani ya uume na kujaa. Kama damu ya kutosha haingii kwenye uume nguvu za kiume pia hupotea. Uume hauwezi kusimama vizuri.
 
HOMONI
Kibaya zaidi ni kwamba kitambi hubadilisha homoni ya kiume iitwayo "testosterone"  kuwa homoni ya kike, "estrogen". Hili hutokeaje? Ni hivi. Mafuta ya kwenye kitambi huzalisha kimeg’enya kiiwatcho aromatase, na hiyo aromatase ndiyo inayobadilisha homoni ya kiume ya testosterone kuwa homoni ya kike estrogen.
 
MISHIPA YA NEVA
Mafuta yaliyo kwenye kitambi hudhuru mishapa laini inayohusika na usimamaji wa uume. Uzito mdogo hata wa shilingi kutokana na mafuta yaliyo kwenye kitambi huweza kudhuru mishipa ya neva inayosimamisha uume.
 
TEZIDUME
Mafuta yaliyo kwenye kitambi pia huaharibu utendaji wa tezidume (prostate gland) kwa sababu uzito wa mafuta hayo huleta shida kwenye tezi hiyo muhimu katika nguvu za kiume.
 
MISULI
Pia uzito wa mafuta ya kwenye kitambi hudhuru misuli iitwayo "pelvic floor muscles". Hii ni misuli muhimu sana, iko chini ya nyonga. Inafanya kazi nyingi, baadhi ya kazi zake ni kusaidia kusimamisha uume kuwa imara kabisa, na pia kuzuia kufika kileleni haraka. Mafuta ya kwenye kitambi huidhikisha na kuidhoofisha misuli hii na hivyo kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.Naam, tumbo lako linaonekana kutuna na kutengeneza mkunjo. Linaonekana kwamba linaweza kuchukua muda mrefu sana kuwa katika hali hiyo, inaweza kuwa miezi au miaka; au linaweza lisiishe kabisa!

matibabu ya uhakika kutoka zephania life herbal clinic

Utaratibu wetu ni kwamba hatumtibu mgonjwa mpaka tufanye mahojiano naye kwa kina juu ya historia ya afya yake kwa ujumla. Kama yuko nje ya Mwanza, tutahojiana naye kwa simu, kama yuko Mwanza basi anaweza kuja moja kwa moja kwenye kliniki yetu. Kama yuko nje ya nchi, tutahojiana naye kwa njia ya email/au WhatsApp.

Kupitia mahojiano hayo ndiyo tunaweza kufahamu chanzo cha tatizo lake, na pia tunaweza kumshauri kufanya vipimo kama tutaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo. Lengo ni kwamba, tunahitaji kumtibu mgonjwa kuanzia chanzo cha tatizo, ni kwa njia hiyo tu ndipo anaweza kupona kabisa tatizo lake.

Matibabu yetu ya kutibu matatizo ya nguvu za kiume humaanisha kwamba; tunatibu matatizo yote yanayosababisha kupungua nguvu za kiume. Tunatibu shida zote zinazoathiri utendaji wa tezidume, tunatibu matatizo ya homoni mwilini, tunatibu tatizo la kufunga choo (constipation) na madhara yaliyoletwa mwilini, tunatibu kabisa kisukari na mtu anapona kabisa, tunatibu kitambi/unene na madhara yake, tunatibu madhara ya kujichua, tunatibu presha ya kupanda na kushuka, tunatibu saratani ya tezidume kabla haijakomaa sana, tunatibu maumivu ya mgongo/kiuno na vyanzo vyake; tunatibu vidonda vya tumbo na mtu anapona kabisa, tunatibu matatizo yote ya moyo, tunatibu presha ya kupanda; tunatibu matatizo ya figo na ini na magonjwa yote ambayo ni sababu ya kupungua nguvu za kiume. 

Hivyo, unapotibu nguvu za kiume, unatibu afya yako kwa ujumla, kinyume na watu wanavyofikiri kwamba labda nguvu za kiume ni ule uume tu!! NGUVU ZA KIUME ZIKO NDANI! Na kuna viungo na vipengele mbalimbali zaidi ya 100 vinavyofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kukupatia nguvu za kiume. Kimojawapo kinaposhindwa kufanya kazi kutokana na maradhi, au vyakula tunavyokula au mtindo wa maisha mbaya na mazingira basi nguvu hupungua. Hivyo tunapotibu nguvu za kiume tunatibu kile kitu kilichosndwa kufanya kazi, na tunatibu ugonjwa uliyopelekea kitu hicho kishindwe kufanya kazi vizuri.

Kwa ushauri na matibabu wasiliana nasi kwa namba za simu:
+255 766 431 675/+255 656 620 725;
WHATSAPP +255 766 431 675
EMAIL: [email protected]

TUNATUMA DAWA MAHALA POPOTE ULIPO

Tunatuma dawa mahala popote mtu alipo ndani na nje ya nchi. Kwa watu walio ndani ya nchi, mzigo huchukua siku 3-5 hadi kukufikia. Na kwa watu walio nje ya nchi mzigo huchukua siku 5-7 ambapo mizigo yote tunatuma kwa DHL; tunavyo vibari vya kusafirisha.

VIDEO| jinsi KUJICHUA kunavyoua nguvu za kiume kabisa

BAADHI YA MAGONJWA NA TABIA ZINAZOATHIRI VIUNGO NA VITU MABALIMBALI MWILINI VINAVYOHUSIKA NA NGUVU za kiume

Kuna tabia na magonjwa mbalimbali zaidi ya 200
ambayo hudhuru viungo na vitu mbalimbali ndani ya mwili vinavyohusika na
nguvu za kiume. Hapa tumekuwekea baadhi ya magonjwa na tabia. Bofya kwenye
maneno "Soma hapa zaidi," uweze kufahamu ni kwa namna gani
ugonjwa husika husababisha kupungua nguvu za kiume.

Picture

KUJICHUA

Kujichua ni tendo linaloua kabisa nguvu za kiume; huvuruga homoni, mishipa ya neva, tezi n.k.
SOMA ZAIDI


Picture

KITAMBI

Kitambi kina madhara mengi kiafya ikiwa ni pamoja na kubadilisha homoni ya kiume kuwa ya kike na hivyo kupunguza nguvu za kiume.
SOMA ZAIDI
Picture

KISUKARI

Kisukari hudhuru mishipa ya damu, mishipa ya neva, homoni, figo n.k, na hivyo kupunguza nguvu za kiume.
​
SOMA ZAIDI
Picture

mishipa ya neva

Ugonjwa unaodhuru mishipa ya neva kama vile Parkinson’s disease, kifafa n.k, hupunguza nguvu za kiume.
​
SOMA ZAIDI
Picture

kufunga choo

 Kusukuma choo kwa nguvu muda mrefu hudhuru misuli iitwayo “Pelvic Floor Muscles” na hivyo kupunguza nguvu za kiume.
​
​SOMA ZAIDI
Picture

matatizo ya ini

Matatizo ya ini husababisha kupungua nguvu za kiume kwa sababu hudhuru utendaji wa baadhi ya homoni mwilini.
​
SOMA ZAIDI
Picture

ngiri

Ngiri hudhuru mishipa ya neva iliyo kwenye uume na  homoni ya testestoron na hivyo kupunguza nguvu za kiume.
SOMA ZAIDI

Picture

presha ya kupanda

 Presha ya kupanda hudhuru mzunguko wa damu, homoni, mishipa ya neva na hivyo kufanya nguvu za kiume kupungua.
SOMA ZAIDI

Picture

uvutaji sigara

Uvutaji wa sigara hudhuru mishipa ya damu ya ateri na hivyo kusababibisha nguvu za kiume kupungua.
SOMA ZAIDI

Picture

baiskeli

Uendeshaji wa basikeli muda mrefu hudhuru mishipa ya neva kwenye korodani na hivyo kupunuguza nguvu za kiume.
SOMA ZAIDI

Picture

upasuaji

Matibabu ya upasuaji huweza kudhuru mishipa ya neva na hivyo kupunuguza nguvu za kiume.
SOMA ZAIDI

Picture

pombe

Pombe huleta mabadiliko makubwa  kwa kuvuruga utendaji wa vitu vingi mwilini na hivyo kupunuguza nguvu za kiume.
SOMA ZAIDI

Picture

viagra

Watu wengi hukurupuka kutumia Viagara na jamii ya Viagara, si tiba kabisa na huchangia sana kuua nguvu za kiume.
SOMA ZAIDI

Picture

tezidume

 Kuvimba kwa tezidume au saratani hudhuru utendaji wa tezi hiyo muhimu na hivyo kupunguza nguvu za kiume.
SOMA ZAIDI

Picture

ULAJI MBAYA

Ulaji mbaya hudhuru na kuharibu utendaji wa mifumo ya mwili, na hivyo kupelekea maradhi mengi na upungufu wa nguvu za kiume.
SOMA ZAIDI
Picture

kuchelewa kulala

Usingizi huchaji upya akili na mwili. Kukosekana kwake hudhoofisha mwili na hivyo kupunguza nguvu za kiume.
SOMA ZAIDI

Picture

msongo wa mawazo

 Msongo wa mawazo ni hatari kwa afya yako. Hupandisha baadhi ya kemikali na kusababisha nguvu za kiume kupungua.
SOMA ZAIDI

Picture

compyuta

Kutumia komputa muda mrefu hupunguza nguvu za kiume kutokana na mionzi, pia kuweka laptop kwenye miguu ni hatari.
SOMA ZAIDI
Picture

vidonda vya tumbo

Vidonda vya tumbo hupunguza nguvu za kiume kwa kudhuru viungo na vitu vinavyohusika na nguvu: vilivyo karibu yake.
SOMA ZAIDI
Picture

mionzi ya simu

Matumizi mabaya ya simu huingiza mionzi mingi mwilini na hivyo kupunguza nguvu za kiume na kudhuru afya zetu.
SOMA ZAIDI
Picture

ukosefu wa mazoezi

Kutofanya mazoezi ni hatari sana kwa afya yako. Mifumo mingi mwilini hudhurika na hivyo nguvu za kiume kupungua.
SOMA ZAIDI
Picture

maumivu ya kiuno

Uti wa mgongo hasa eneo la kiuno ndiyo kituo kikuu. Shida yoyote kwenye eneo hilo hupunguza nguvu za kiume.
SOMA ZAIDI
Picture

magonjwa ya figo

 Figo zina mchango muhimu sana katika nguvu za kiume. Shida yoyote katika figo husababisha nguvu za kiume kupungua.
SOMA ZAIDI
Picture

matatizo ya homoni

Matatizo ya kihomoni ndani ya mwili ni sababu kubwa kwa wanaume wengi kupungukiwa nguvu za kiume.
SOMA ZAIDI 

MAKALA MAALUMU

Je, wewe umewahi kujichua?Usiache kusoma hapa.
​

dawa zetu ni za

Asili
Dawa zetu zinatokana na mimea tiba na matunda kutokana na miti ambayo imethibitika kisayansi kuwa ina uwezo wa mkubwa wa kutibu matatizo mbalimbali ya kiafya ikiwa ni pamoja na matatizo ya nguvu za kiume kwa uhakika mkubwa.

kuthibitishwa kwa

Mkemia
Kwa kuwa tumejikita katika kuhudumia wagonjwa kwa matibabu ya uhakika; baadhi ya dawa zetu nyingi zimepimwa na kuthibitishwa na Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa ni nzuri hazina madhara yoyote.  Na zingine ziko kwenye mchakato.

matibabu yetu ni

Uhakika
Matibabu yetu ni ya uhakika, si ya kubahatisha. Tunatibu hadi mgonjwa apone kabisa. Tunatibu kuanzia chanzo cha tatizo. Tunamtibu mgonjwa mahala popote alipo ndani na nje ya nchi. Usipopona unarudishiwa nusu ya gharama au yote.

BAADHI YA DAWA ZETU

Zifuatazo ni baadhi ya dawa zetu zinazotibu nguvu za kiume kwa uhakika mkubwa sana
Picture

BODY COMPLEX

Inarekebisha mifumo ya mwili, na kutibu magonjwa mengi.
SOMA ZAIDI
Picture

BALIJAAM

Inatibu uregevu wa uume na kufika haraka kileleni.
SOMA ZAIDI
Picture

EXPORERE

Inaimarisha stamina ya mwili na kukufanya urudie zaidi.
SOMA ZAIDI
DAWA YA UHAKIKA YA KUZUIA KUFIKA HARAKA KILELENI

magonjwa mengine tunayotibu kwa uhakika mkubwa

Picture

matatizo ya ngozi

Picture

pumu

Picture

saratani

DAWA YA UHAKIKA YA KUZUIA KUFIKA HARAKA KILELENI
Picture

matatizo ya HEDHI

Picture

BAWASILI

Picture

BARIDI YABISA

DAWA YA UHAKIKA YA KISUKARI. IMEPIMWA NA
KUTHIBITISHWA NA MKEMIA MKUU WA SERIKALI.

MAELEZO ZAIDI BOFYA HAPA

DAWA YA UHAKIKA YA KUZUIA KUFIKA HARAKA KILELENI
Picture

sickle-cell

Picture

fangasi za ukeni

Picture

kipanda uso

Picture
Dr. Khamisi Ibrahim Zephania ni daktari bingwa aliyebobea
katika kutibu matatizo ya nguvu za kiume na magonjwa sugu. Anatibu
hadi tatizo lako liishe kabisa. Ni matibabu
ya uhakika wala si ya kubahatisha.
+255 766 431 675/+255 656 620 725

WHATSAPP: +255 766 431 675
EMAIL: [email protected]

ONYO: Ni marufuku kunakili makala hizi, hatua kali za kisheria zitachukuliwa. Baadhi ya watu wana tabia ya "kukopi" na "kupesti" masomo haya kisha kutupia kwenye blogu zao na kujifanya wanaweza kutibu matatizo ya nguvu za kiume ilihali hawawezi chochote. Kutibu upungufu wa nguvu za kiume sio rahisi vile watu wanavyofikiri. Inahitaji utaalamu na ubobezi wa hali ya juu sana katika mfumo wa uzazi wa mwanamume. Sio kubugia dawa tu. Nawe mgonjwa kuwa makini sana; epuka kutapiliwa.

SOMA ZAIDI MAKALA ZETU ZINGINE....

>>Umuhimu wa vitamini D kwa nguvu za kiume...
>>Dawa sahihi ya kutibu ugonjwa wa kisukari...
>>Dawa za kusimamisha uume kama msumari....
>>Ugonjwa wa ngiri na tiba yake...
>>Madhara ya kitambi kwa nguvu za kiume...
>>Matibabu ya uhakika ya nguvu za kiume..
>>Tambua jinsi nguvu za kiume zinavyotibiwa kitaalamu
>>Jinsi maji yanavyorudisha nguvu za kiume
>>Jinsi nguvu za kiume zinavyotibiwa kitaalamu
>>Dawa na matibabu sahihi ya vidonda vya tumbo

>>Dawa na matibabu sahihi ya fangasi
>>Dawa na matibabu sahihi ya kuondoa sumu mwilini
>>Dawa na matibabu sahihi ya chunusi
>>Matibabu ya Saratani ya kibofu cha mkojo

>>Dawa nzuri ya asili ya saratani ya mifupa
>>Matibabu ya asili ya uvimbe kwenye ubongo
>>Matibabu ya asili ya saratani ya matiti kwa wanawake
>>Matibabu ya asili ya saratani ya matiti kwa wanaume
>>Kutanuka zaidi kwa njia za hewa za mapafu

PEPTICA

DAWA YA ASILI YA VIDONDA VYA TUMBO

Peptica - dawa ya vidonda vya tumbo
INATIBU NA KUMALIZA KABISHA VIDONDA VYA TUMBO VYA AINA ZOTE. MAELEZO ZAIDI BOFYA HAPA

KWA USHAURI NA MATIBABU, KUAGIZA DAWA, kuripoti
maendeleo yako UNAWEZA KUWASILIANA NASI
POPOTE ULIPO, TUTAKUFIKIA.

BOFYA HAPA

Zephania Life Herbal Clinic


Hours

M-F: 7am - 9pm

Telephone

+255 766 431 675
+255 656 620 725

Email

[email protected]
  • Home
    • Home - Eng
  • About
  • Service
  • Contact
  • Kipanda Uso, Sababu, Dalili Na Matibabu Sahihi
  • Hatari Za Kiafya Za Uzito Mkubwa Na Tiba Yake
  • Dawa ya Asili ya Bawasiri
  • ujuh
  • Pumu (Asthima): Sababu, Dalili, na Tiba Asili Iliyothibitishwa Kisayansi
  • BAWESI: Natural Hemorrhoid Remedy for Internal & External Healing