Maumivu ya kiuno
Maumivu ya kiuno (kwa Kiingereza: lumbago) ni hali inayotokea mara nyingi na inayohusu misuli na mifupa ya upande wa chini wa mgongo. Hali hii huathiri takriban 40% ya watu kwa wakati fulani maishani mwao.
Maumivu ya kiuno yanaweza kuainishwa kwa urefu kama maumivu makali ya ghafla (yanayodumu kwa kipindi cha chini ya wiki 6), maumivu sugu ya wastani (wiki 6 hadi 12), au maumivu sugu (zaidi ya wiki 12). Hali hii pia inaweza kuainishwa kulingana na visababishi kama inasababishwa na jeraha au sivyo au maumivu hame.
Katika visa vingi vya maumivu ya kiuno, kisababishi kikuu maalumu hakitambuliwi wala kukisiwa, kwa kuwa maumivu huaminika kutokana na jeraha kama vile mkazo wa misuli au mkazo wa viunga. Ikiwa maumivu hayaponi baada ya kutibiwa kwa njia isiyohusisha upasuaji au ikiwa maumivu yataandamana na "tahadhari" kama vile kupungua uzito bila sababu, homa, au matatizo makuu ya kihisia au mwendo, uchunguzi zaidi unaweza kuhitajika kubaini kisababishi kikuu.
Mara nyingi, vifaa vya utambuzi kama vile tomografia iliyohasibiwa kwa eksirei havihitajiki navyo huandamana na hatari zake. Licha ya athari hizi, matumizi ya pichatiba kuchunguza maumivu ya kiuno yameongezeka.
Baadhi ya maumivu ya kiuno husababishwa na kuharibika kwa diski za baina ya pingili za uti wa mgongo, na uchunguzi wa kunyoosha mguu ni muhimu katika kubaini visa hivyo.
Katika watu wenye maumivu sugu, mfumo wa mwili unaochakata maumivu unaweza kutofanya kazi vyema, hivyo kusababisha maumivu makali ukijaribu kujibiza shughuli zisizo na hatari kubwa.
Matibabu ya maumivu ya ghafla ya kiuno kwa kawaida huwa haihusishi upasuaji, kama vile vituliza maumivu na kuendeleza kazi za kawaida jinsi mtu anavyoweza licha ya maumivu. Matibabu hupendekezwa kwa kipindi ambapo yanamsaidia mtu, huku dawa aina ya acetaminophen (inayojulikana pia kama paracetamol) ni ya kwanza kupendekezwa. Dalili za maumivu ya kiuno hufifia baada ya wiki chache, huku 40 - 90% ya watu wakipata nafuu kabisa baada ya wiki sita.
Kuna njia nyingi mbadala katika watu wasiopata nafuu baada ya matibabu ya kawaida. Opioidi zinaweza kusaidia ikiwa vituliza maumivu vya kawaida havitafaulu, ingawa kwa jumla hazipendekezwi kwa sababu zina madhara, hasa uraibu. Upasuaji unaweza kuwafaidisha watu wenye matatizo ya maumivu sugu na ulemavu unaohusiana na diski.Upasuaji pia unaweza kuwafaidisha watu wenye stenosisi ya uti wa mgongo. Hakuna manufaa bayana ya upasuaji yaliyopatikana kwa visa vingine vya maumivu ya kiuno yasiyo na kisababishi cha moja kwa moja.
Isitoshe, kuna matibabu ya dawa mbadala, ambayo ni pamoja na mbinu ya Alexander na mitishamba, lakini hakuna ushahidi wa kutosha kupendekeza matibabu hayo kikamilifu. Ushahidi wa utunzaji wa tibamwili na kunyooshaji uti wa mgongo umekumbwa na utata.
Maumivu ya kiuno mara nyingi huathiri hisia, tatizo linaloweza kuimarishwa kupitia ushauri wa kisaikolojia na/au dawa za kushusha utendakazi.
Ishara na daliliKatika dalili za kawaida za maumivu ya kiuno, maumivu huanza baada ya mwendo wa kunyanyua vitu, kujipinda au kuinama. Dalili za hali hii zinaweza kuanza baada ya mwendo wowote au mtu anapoamka asubuhi inayofuata. Maelezo ya dalili hizi yanaweza kuwa maumivu katika sehemu fulani au maumivu yanayosambaa. Maumivu yanaweza kutokuwa makali kufuatia shughuli, kama vile kuinua miguu, au hali nyingine kama kuketi au kusimama. Maumivu yanayosambaa chini ya miguu (yanayojulikana kama maumivu ya nyonga) yanaweza kuwepo.
Visa vya kwanza vya maumivu makali ya ghafla ya mgongo huanza katika umri wa miaka 20-40. Mara nyingi kisa hicho huwa ni sababu ya kwanza katika watu wazima kumwona daktari.[1] Kisa hicho hurejea katika zaidi ya nusu ya waathiriwa[2] huku kisa cha kurejea kikiandamana na maumivu makubwa kuliko kisa cha kwanza.[1]
Matatizo mengine yanaweza kuandamana na maumivu ya kiuno. Maumivu sugu ya kiuno huhusishwa na matatizo ya usingizi, ikiwa ni pamoja na wakati mwingi unaohitajika kulala, kusumbuka wakati wa kulala, kulala kwa kipindi kifupi, na kutotosheka na usingizi.[3] Isitoshe, idadi kubwa ya watu wenye maumivu sugu ya kiuno huonyesha dalili za mfadhaiko[4] au wasiwasi.[5]
KisababishiMaumivu ya kiuno si ugonjwa, bali ni hali inayoweza kusababishwa na matatizo mengi yanayotofautiana kwa kiwango na hatari.[6] Visa vingi vya maumivu ya mgongo havina kisababishi maalum[1] ingawa vinaaminika kutokana na masuala ya misuli au mifupa kama vile kuteguka au mkazo wa misuli.[7]
Unene wa kupindukia, kuvuta sigara, kunenepa wakati wa ujauzito, mfadhaiko, matatizo ya mwili, mkao mbaya na kulala vibaya pia huchangia maumivu ya kiuno. [7] Orodha ya visababishi vyenye uwezekano wa kusababisha maumivu ya kiuno ni pamoja na hali zisizotokea mara nyingi.[8] Matatizo ya kimwili yanaweza kuwa osteoathritisi, athritisi ya rumatoidi, kuharibika kwa diski zilizo katikati mwa pingili za uti wa mgongo au henia ya diski ya uti wa mgongo, kuvunjika kwa pingili za uti wa mgongo (kama vile kufuatia osteoporosisi) au, kwa nadra, maambukizi au tyuma ya uti wa mgongo.[9]
Wanawake wanaweza kuwa na maumivu ya kiuno kutokana na hali zinazoathiri mfumo wa uzazi, ikijumuisha endometriosisi, sisti ya ovari, saratani ya ovari au fibroidi ya uterasi.[10] Karibu nusu ya wanawake wajawazito hulalamikia maumivu ya kiuno au ya sehemu ya sakramu wakati wa ujauzito, kufuatia mabadiliko ya hali ya kukaa na kiuo cha mvuto hivyo kusababisha mkazo wa misuli na kano.[11]
PathofiziolojiaMiundo ya mgongo
The five lumbar vertebrae define the lower back regionThe structures surrounding and supporting the vertebrae can be sources of low back painSehemu ya kiuno ina pingili tano (L1-L5). Baina ya pingili za uti wa mgongo kuna diski zenye gegedu na nyuzi, ambazo huzuia pingili zisikwaruzane, na pia kuukinga uti wa ubongo. Neva hutoka na kuingia katika uti wa ubongo kupitia vitundu maalum baina ya pingili, zikituma hisia na arifa kwenye ngozi na misuli. Uthabiti wa uti wa mgongo huchangiwa na kano na misuli ya mgongo na ya fumbatio. Viunga vidogo vinavyoitwa viunga vya zigapofizi huthibiti na kuelekeza mwendo wa uti wa mgongo.[12]
Misuli ya nyuzi nyingi hupanda na kushuka katika sehemu ya nyuma ya uti wa mgongo, na ni muhimu kwa kuwa hunyoosha uti wa mgongo na kuuimarisha wakati wa miendo kama vile kuketi, kutembea na kunyanyua vitu.[13]. Mara nyingi tatizo la misuli hii hupatikana katika watu wenye maumivu sugu ya kiuno, kwa sababu maumivu haya husababisha mtu kutumia misuli ya mgongo vibaya katika harakati ya kuepuka maumivu.[14] Tatizo la hali ya misuli yenye nyuzi nyingi huendelea hata baada ya maumivu kutulia, hivyo huenda ni kisababishi kikuu cha kurejea kwa maumivu.[14] Inapendekezwa kuwafunza watu wenye maumivu sugu ya kiuno jinsi ya kutumia misuli hii kama njia ya matibabu.[14]
Diski ya baina ya pingili za uti wa mgongo ina kitovu cha jelatini kilichozingirwa na kizingo cha nyuzi.[15] Katika hali ya kawaida, bila jeraha, sehemu kubwa ya diski hii haihuishwi na mfumo wa usafirishaji wala mfumo wa neva – damu na neva hupitia nje ya diski tu.[15] Seli maalum zinazoweza kuishi bila kupata damu ya moja kwa moja huwa ndani ya diski.[15]
Wakati unapopita, diski huwa ngumu na kukosa uwezo wa kuhimili shinikizo.[6] Hali hii ya diski kukosa kuhimili shinnikizo huongeza shinikizo kwenye sehemu zingine za uti wa mgongo, hivyo kusababisha kano ya uti wa mgongo kuwa nene na pia vifundo vya mfupa kukua kwenye pingili.[6] Kufuatia hali hii, kutakuwepo na nafasi ndogo ambapo uti wa ubongo na mizizi ya neva itaweza kupitia.[6] Diski inapoharibika kufuatia jeraha au ugonjwa; muundo wake hubadilika: mishipa ya damu na neva zinaweza kuingia ndani ya diski na/au hania ya diski zinaweza kuifinya mizizi ya neva.[15] Mabadiliko yoyote haya yanaweza kusababisha maumivu ya mgongo.[15]
Hisia za maumivuKwa jumla, maumivu ni hisia isiyopendeza inayokujibiza tukio linaloharibu au linaloweza kuharibu tishu za mwili. Kuna hatua tatu kuu katika utaratibu wa kuhisi maumivu: uhamishaji, usambazaji,hisia, na ubadilishaji kwa kutumia neva.[13] Seli za neva zinazotambua maumivu zina miili kwenye kikundi cha seli za shina la uti wa mgongo na nyuzi zinazosambaza arifa za neva hadi kwenye uti wa ubongo.[16]
Utaratibu wa kuhisi maumivu huanza tukio lililosababisha maumivu linapochochea ncha za seli za neva za hisia. Seli hii hubadilisha tukio la maumivu kuwa vimuli vya umeme kwa njia ya uhamishaji. Aina mbalimbali za nyuzi za neva husambaza arifa za umeme kutoka kwenye seli zinazotekeleza uhamishaji hadi pembe ya nyuma ya uti wa mgongo. Kutoka hapa, arifa huelekezwa kwenye shina la ubongo, kisha kutoka kwenye shina la ubongo hadi sehemu mbalimbali za ubongo kama vile thalamasi na mfumo wa viungo. Katika ubongo, arifa za maumivu huchakatwa na kuainishwa katika utaratibu wa hisia ya maumivu. Kupitia njia ya uhamishaji, ubongo unaweza kubadilisha jinsi ya kusambaza arifa za neva kwa kupunguza au kuongeza utoaji wa nyurotransmita.[13]
Sehemu za mfumo wa hisia na utaratibu wa maumivu zinaweza kukosa kufanya kazi kama kawaida; hivyo kusababisha hisia ya maumivu, hata kukiwa hakuna kisababishi chochote nje ya mwili, na kuashiria maumivu makali kutoka kisababishi maalum, au kuashiria maumivu kutoka tukio ambalo kwa kawaida halisababishi maumivu. Isitoshe, utaratibu wa ubadilishaji wa maumivu unaweza kukosa kufanya kazi kama kawaida. Matukio haya huhusika na maumivu sugu.[13]
UtambuziUainishajiKuna njia mbalimbali za kuainisha maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo.[8] Kwa kijumla, kuna aina tatu za maumivu ya mgongo, zikiainishwa kulingana na visababishi: Maumivu ya mgongo kufuatia jeraha (hii ni pamoja na mikazo ya misuli na mifupa isiyo na kisababishi bayana, hania ya diski, kufinywa kwa mizizi ya neva, diski zilizoharibika au ugonjwa wa viunga, na kuvunjika kwa pingili za uti wa mgongo), maumivu ya mgongo yasiyohusiana na jeraha (saratani, hali za inflamesheni spondiliathritisi, na maambukizi), na maumivu hamekutoka viungo vya ndani (magonjwa ya kibofu na nyongo, jiwe la figo, maambukizi ya figo, na aneurisimi ya aota, miongoni mwa matatizo mengine).[8] Matatizo yanayohusiana na jeraha au misuli na mifupa huchangia visa vingi (takriban 90% au zaidi),[8][17]. Kati ya visa hivi, visa vingi (karibu 75%) havina kisababishi maalum kilichobainishwa, lakini huaminiwa kutokana na mkazo wa misuli au jeraha la kano.[8][17] Mara nadra, visa vya maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo hutokea kufuatia matatizo ya mifumo ya mwili na ya kisaikolojia, kama vile fibromialgia na tatizo la somatofomu.[17]Maumivu ya kiuno yanaweza kuainishwa kulingana na ishara na dalili. Maumivu enezi yasiyobadilika kufuatia mwendo wowote wa mwili, huhisiwa tu kwenye sehemu ya chini ya mgongo bila kuenea aidi ya matako, huainishwa kama yasiyo na kisababishi maalum, ambayo ni aina ya maumivu yanayotokea mara nyingi.[8] Maumivu yanayoenea kuelekea miguuni chini ya goti huwa katika sehemu moja (katika hania ya diski), au katika sehemu zote mbili (katika stenosisi ya uti wa mgongo), na yanayobadilika kwa uchungu kufuatia miendo fulani ya mwili huainishwa kama enezi. Maumivu haya huchangia 7% ya visa.[8] Maumivu yanayoandamana na matatizo makali kama vile jeraha, homa, historia ya saratani au ulegevu mkuu wa misuli na matatizo mengine andamizi huainishwa kama yanayohitaji kushugulikiwa kwa dharura.[8]
Dalili pia zinaweza kuainishwa kulingana na muda, kama vile maumivu makali, maumivu sugu kidogo (pia yanayojulikana kama maumivu makali kidogo), au maumivu sugu. Kipindi maalum kinachohitajika ili kutambua kila mojawapo ya aina hizi za maumivu hakijabainishwa kikamilifu, lakini kwa kijumla, maumivu yanayodumu chini ya wiki sita huainishwa kama maumivu makali ya ghafla. Maumivu yanayodumu kati ya wiki sita hadi kumi na mbili ni maumivu sugu kidogo , ilhali maumivu ya zaidi ya wiki kumi na mbili ni maumivu sugu.[18] Udhibithi na utambuzi unaweza kubadilika kulingana na kipindi cha dalili.
TahadhariDalili hatari huashiria matatizo makaliRed flag[19]Vipengele vinavyowezekana kuwa visababishi[1]
Historia ya sarataniSaratani
Kupoteza uzito bila sababu
Kupoteza uwezo wa kudhibiti kibofu au kinyweoKauda
ekuina
sindromu
Udhaifu mkuu wa misuli
au ukosefu wa hisia
Kukosa hisia kwenye
matako (anestesia ya makalio)
Jeraha kubwa ikilinganishwa na umriMvunjiko
Matumizi ya steroidi za ubongo kwa muda mrefu
Maumivu makali kufuatia
upasuaji wa kiunoni mwaka uliotanguliaMaambukizi
Homa
Maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo
Ushinikizaji wa mfumo wa kingamwili
Kutumia dawa za kudungia mishipaniKwa kuwa muundo wa mgongo ni tata, na njia ya kuripoti kuhusu maumivu ni yenye uvumi na huathiriwa na vipengele vya kijamii, utambuzi wa maumivvu ya sehemu ya chini ya mgongo si dhahiri.[8] Huku idadi kubwa ya maumivu ya mgongo yakisababishwa na matatizo ya misuli na viunga, visababishi hivi vinapaswa kutofautishwa na matatizo ya kineva, tyuma za uti wa mgongo, mvunjiko katika uti wa mgongo na maambukizi, miongoni mwa matatizo mengine.[1][18] Uwepo wa dalili fulani zinazojulikana kama tahadhari, huashiria haja ya uchunguzi zaidi ili kutathmini matatizo mengine andamizi yanayoweza kuhitaji matibabu maalum au ya dharura.[8] Uwepo wa dalili hatari haumaamishi kuna tatizo kuu. Dalili hizi ni kidokezo tu,[20][21] na watu wengi wenye tahadhari hizi huwa hawana tatizo lolote andamizi la kuhatarisha maisha.[1][18]Bila dalili hatari, kufanya uchunguzi wa pichatiba au uchunguzi wa maabarani katika wiki nne za kwanza baada ya dalili kutokea hakujathibitishwa kuwa na umuhimu wowote.[8] Baada ya sababu zingine kuondolewa, watu wenye maumivu yasiyo na kisababishi bayana hupewa matibabu ya kutuliza dalili.[1][18] Jitihada za kugundua vipengele vinavyoweza kutatiza utambuzi, kama vile mfadhaiko, matumizi mabaya ya dawa, au swala kuhusu malipo ya bima, zinaweza kuwa na manufaa[8]
Uchunguzi
The straight leg raise test can detect pain originating from a herniated disc. When warranted, imaging such as MRI can provide clear detail about disc related causes of back pain (L4–L5 disc herniation shown)Uchunguzi wa pichatiba hupendekezwa panapokuwa na tahadhari, mfululizo wa dalili za kineva zisizopona, au maumivu yanayoendelea au yanayozidi kuwa makali.[8] Hususan, kutumia uchunguzi wa pichatiba mapema(Picha wa Mwangwi wa Sumaku au CT) hupendekezwa katika visa vinavyoshukiwa kuwa saratani, maambukizi, ausindromu ya kauda ekuina.[8] Picha wa Mwangwi wa Sumaku ni bora kidogo kuliko Tomografia ya Kompyuta katika kutambua ugonjwa wa diski. Mbinu hizi mbili ni muhimu katika utambuzi wa stenosisi ya uti wa mgongo.[8] Ni vipimo vichache tu vya kimwili vinavyosaidia.[8] Uchunguzi wa kunyoosha miguu mara nyingi huwanufaisha watu wenye hania wa diski.[8] Uchunguzi wa diskografi ya kiuno unaweza kusaidia kubainisha diski maaluum inayosababisha maumivu katika watu wenye maumivu sugu ya kiwango cha juu.[22] Vile vile, taratibu za kimatibabu kama vile kuziba neva zinaweza kutumika ili kubaini kiini maalum cha maumivu.[8] Tafiti zingine hupendekeza matumizi yakudunga sehemu za viunga, kudunga epidura kwenye trasfomina na kudunga sakramu na iliamu kama njia ya kufanya utambuzi[8] Uchunguzi mwingine wa kimwili kama vile kutathmini skoliosisi, ulegevu au uelemavu wa misuli, hitilafu ya msisimko wa misuli,si muhimu sana.[8]Maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo ni mojawapo ya sababu zinazofanya watu watafute usaidizi wa daktari.[23][24] Katika maumivu yaliyodumu kwa wiki chache tu, kuna uwezekano wa maumivu kutulia bila matibabu.[25] Hivyo, ikiwahistoria ya kimatibabu naUchunguzi wa mwili wa mtu hazitabaini ugonjwa fulani kuwa kisababishi, jamii za madaktari hazipendekezi uchunguzi kama vile eksirei, uchunguzi wa Tomografia ya Kompyuta, na Picha za Mwangwi wa Sumaku.[24] Mgonjwa anaweza kuagiza kufanyiwa uchunguzi huo, lakini utafanywa tu ikiwa kuna dalili hatari ,[26][27] uchunguzi huu ni huduma za afya zisizohitajika.[23][25] Uchunguzi wa pichatiba huongeza gharama, na huhusika kwa kiwango kikubwa na upasuaji usio na manufaa ya kijumla, [28][29]na minunurisho inayotumika inaweza kudhuru afya ya mgonjwa.[28] Chini ya 1% ya vipimo vya pichatiba chini hubaini kisababishi cha tatizo hili.[23] Kupitia uchunguzi wa picha tiba, hitilafu zingine za kimwili zisizodhuru mwili zinaweza kugunduliwa, jambo linaloweza kusababisha watu waagize uchunguzi mwengine usiohitajika au kuingiwa na wasi wasi.[23] Hata hivyo, uchunguzi wa Picha wa Mwangwi wa Sumaku kwenye kiuno uliongezeka kwa zaidi ya 300% miongoni mwa watu walionufaika na huduma ya Medicare nchini Marekani mwaka wa 1994 hadi 2006.[30]
KingaNjia bora za kuzuia maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo hazijakuzwa kikamilifu.[31] Mazoezi ni muhimu hasa katika kuzuia kurejea kwa maumivu katika watu walioathiriwa kwa zaidi ya wiki sita.[1][32] Gondoro zenye uthabiti wastani ni bora zaidi katika watu wenye maumivu sugu kuliko gondoro ngumu.[33] Kuna ushahidi mdogo unaoonyesha kuwa mishipi ya mgongo ina manufaa mengi katika kuzuia maumivu ya mgongo kuliko kuwaelimisha watu kuhusu mbinu bora za kunyanyua vitu.[34] Soli ya ndani ya viatu haisaidii kuzuia maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo.[35]
UdhibitiUdhibiti wa maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo hutegemea ni kipi kati ya vipengele hivi kilichosababisha hali hii: matatizo yanayohusiana na jeraha, matatizo yasiyohusiana na jeraha, au maumivu hame.[36] Katika visa vya maumivu makali ya ghafla yanayosababisha matatizo hafifu hadi ya wastani, lengo la matibabu ni kurejesha utendakazi wa mwili hadi hali ya kawaida, na kupunguza maumivu. Kwa kawaida, hali hii si hatari kwa sababu husuluhika bila matibabu mengi na kupona kwake huwezeshwa na jaribio la kurejesha shughuli za kawaida haraka iwezekanavyo jinsi maumivu yanavyoruhusu.[18] Kuwapa wagonjwa stadi za kujikimu kupitia kuwahimiza kuhusu ukweli huu ni muhimu katika kuharakisha utaratibu wa kupata nafuu.[1] Katika watu wenye maumivu sugu kidogo na maumivu sugu, matibabu kutoka kwa wahudumu wa taaluma mbalimbali yanaweza kuwasaidia.[37]
Udhibiti wa mwiliImependekezwa kuongeza mazoezi ya kijumla ya mwili, lakini hakuna uhusiano bayana uliotambulika kati ya mazoezi haya na maumivu au ulemavu yanapotumika kama matibabu ya maumivu ya ghafla.[32][38] Tafiti za kiwango cha chini hadi za kiwango cha juu zimependekeza kutembea kama njia ya kutibu maumivu ya ghafla.[39] Kulingana na Mbinu ya McKenzie kutibu maumivu ya mgongo ni bora kidogo katika kutibu maumivu ya ghafla ya mgongo, lakini manufaa yake ya muda mfupi hayajaonekana kufaulu kikamilifu.[1] Kuna ushahidi wa kutosha unaopendekeza matumizi ya tibajoto kwa maumivu ya mgongo ya ghafla na maumivu sugu kidogo[40] lakini kuna ushahidi mdogo unaopendekeza matumizi ya tibabaridi au tibajoto kwa maumivu sugu.[41] Ushahidi dhaifu unapendekeza kuwa mishipi ya kiunoni inaweza kuongeza idadi ya siku za kwenda kazini, ingawa hakuna ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa itasaidia kupunguza maumivu.[34] Matibabu ya sauti kuu na wimbi la sauti hayajatambulika kufaulu, hivyo hayapendekezwi.[42]Matibabu ya mazoezi ni bora katika kupunguza maumivu na kuimarisha utendakazi wa mwili katika watu wenye maumivu sugu ya mgongo[34] Mazoezi pia yametambulika kupunguza uwezekano wa maumivu kurejea kwa kipindi cha hadi miezi sita baada ya kukamilisha tiba hii ya mazoezi[43] na pia kuimarisha utendakazi wa kudumu.[41] Hakuna uhahika kuwa aina moja ya tiba ya mazoezi ni bora kuliko nyingine.[44] Mbinu ya Alexander imekisiwa kufaulu katika kutibu maumivu sugu ya mgongo,[45] na kuna ushahidi wa kutosha unaopendekeza matumizi ya yoga.[46] Kusisimua neva kupitia ngozi hakujatambulika kufaulu katika kutibu maumivu sugu ya mgongo.[47] Utafiti kuhusu matumizi ya soli za ndani za viatu haujatamatishwa.[35] Mchangamsho wa neva za pembeni, utaratibu wenye viwango vya chini vya uvamizi neva, ni matibabu yanayoweza kufaulu kwa visa vya maumivu sugu yasiyotibika kwa matibabu mengine, ingawa utafiti unaopendekeza hatua hii haujakamilika, na si bora kwa maumivu yanayosambaa miguuni.[48]
DawaUdhibiti wa maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo mara nyingi huhusisha kutumia dawa kwa kipindi ambacho zinafanikisha. Katika kutibu kisa cha kwanza cha maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo, malengo makuu ni kupata nafuu kabisa. Hata hivyo, ikiwa tatizo litakuwa sugu, lengo linaweza kubadilika kuwa kudhibiti maumivu na kurejesha utendakazi wa mwili haraka iwezekanavyo. Kwa kuwa dawa za kutuliza maumivu ni bora kwa kiasi fulani, malengo ya manufaa ya dawa hizi yanaweza kutofautiana na matokeo halisia, jambo linaloweza kupunguza utoshelezaji.[4]Kwa kawaida, dawa inayopendekezwa mara ya kwanza niacetaminophen audawa za kuzuia inflamesheni zisizo na steroidi (wala si aspirini), na dawa hizi huwafaa watu wengi. Kipimo cha acetaminophen kinachokubalika huwa ni salama; ingawa kipimo cha juu kinaweza kusababisha matatizo ya ini.[4] Dawa za kuzuia inflamesheni zisizo na steroidi ni bora katika kutibu maumivu ya ghafla kuliko acetaminophen. Hata hivyo, kuna hatari kubwa ya kusababisha madhara, ikijumuisha: matatizo ya mafigo, vidonda vya tumbo na uwezekano wa matatizo ya moyo. Hivyo, dawa za kuzuia inflamesheni zisozo na steroidi ni chaguo la pili baada ya acetaminophen, inayopendekezwa tu iwapo maumivu hayakushughulikiwa mapema. Dawa za kuzuia inflamesheni zisizo na steroidi hunapatikana katika aina mbalimbali; hakuna utafiti unaopendekeza kutumiakizuizi cha COX-2 kuliko aina yoyote ya dawa ya kuzuia inflamesheni kwa msingi wa manufaa yake.[4] Kwa msingi wa usalama, dawa aina ya naproxen inaweza kuwa bora zaidi.[49] Kilainisha misuli pia kinaweza kunufaisha.[4]Ikiwa maumivu yangali hayajathibitiwa, oipioidikama vile morphine inaweza kutumiwa. Dawa hizi zina hatari ya kusababisha uraibu, na zinaweza kukosa kuchangamana na dawa zingine. Dawa hizi pia zina hatari kubwa ya kusababisha madhara, kama vile kizunguzungu, kichefuchefu, na uyabisi wa utumbo. Opioidi zinaweza kufaa kwa udhibiti wa maumivu makali ya ghafla yanayosababisha matatizo makuu.[4] Makundi ya wataalamu wameshauri dhidi ya matumizi ya muda mrefu ya opioidi kutibu maumivu sugu ya mgongo.[4] Katika watu wazee wenye maumivu sugu, opioidi zinaweza kutumika katika wale wanaoathiriwa vibaya na dawa ya kuzuia inflamesheni zisizo na steroidi, kama vile watu wenye kisukari, matatizo ya tumbo au moyo. Opioidi pia zinaweza kuwa kukinufaisha kikundi fulani cha watu wenyemaumivu ya neva.[50]Dawa ya kutuliza mfadhaikoinaweza kuwa bora katika kutibu maumivu sugu yenye dalili zinazohusiana na mfadhaiko, lakini ina hatari ya kusababisha madhara. Ingawa dawa za kutuliza tukutiko, gabapentin na carbamazepine, wakati mwingine hutumika kutibu maumivu sugu na zinaweza kutuliza maumivu ya nyonga, hakuna ushahidi wa kutosha kupendekeza matumizi yake.[4] Steroidi za kumeza hazijathibitishwa kufaulu kutibu maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo.[1][4] Kudunga sehemu ya viunga na kudunga steroidi kwenye diski hakujatibithishwa kuwanufaisha watu wenye maumivu sugu na yasiyosambaa. Hata hivyo, taratibu hizi zinaweza kupendekezwa katika watu wenye maumivu ya nyonga yanayoendelea.[51] Kudunga steroidi za ubongo kwenyeEpidura huimarisha afya, japo kwa muda mfupi kwa njia inayotiliwa shaka katika watu wenye maumivu ya nyonga, lakini hakuna manufaa ya kudumu.[52]
UpasuajiUpasuaji unaweza kufaa katika watu wenye hania ya diski inayosababisha maumivu makali yanayosambaa miguuni, udhaifu mkuu wa misuli ya miguu, matatizo ya kibofu au kushindwa kuthibiti kinyesi.[53] Upasuaji pia unaweza kufaa katika watu wenye stenosisi ya uti wa mgongo.[54] Katika visa ambavyo maswala haya hayapo, hakuna ushahidi wa kutosha kuthibisha manufaa ya upasuaji.[53]Utolewaji wa diski (Kutoa sehemu ya diski inayosababisha maumivu ya mguu) unaweza kutuliza maumivu haraka kuliko matibabu yasiyohusisha upasuaji.[53] Utolewaji wa diski hupelekea matokeo bora ukifanywa mwaka wa kwanza, lakini si mwaka wa nne hadi kumi.[53] Utolewaji wa diski usioingia ndani sana utolewaji kadri wa diski haujathibitishwa kusababisha matokeo tofauti kuliko utolewaji wa kawaida wa diski.[53] Katika hali zingine nyingi, hakuna thibitisho la kutosha kupendekeza upasuaji.[53] Si bayana athari ya kudumu ulio nao upasuaji dhidi ya kuharibika kwa diski.[53] Upasuaji usioingia ndani ya diski sana hupona haraka, lakini utafiti kuhusu ubora wake hautoshi.[53]
Katika watu wenye maumivu yanayohisiwa kwenye sehemu ya chini ya mgongo pekee kufuatia kuharibika kwa diski, utafiti wa kuaminika umependekezauunganishaji mifupa ya uti wa mgongo kuwa sawa na mazoezi mazito, na bora kidogo kuliko hatua nyepesi zisizohusisha upasuaji.[54] Uunganishaji mifupa ya uti wa mgongo unaweza kupendekezwa katika watu wenye maumivu ya mgongo kufuatiahali pokezi ya kuhama kwa pingili kwa sababu hali hii haiimariki kwa kutumia matibabu yasiyohusisha upasuaji.[53] Hata hivyo, ni wachache tu katika watu waliofanyiwa upasuaji wa kuunganisha mifupa ya uti wa mgongo wanaopata matokeo bora.[54] Kuna taratibu nyingi za upasuaji ili kuunganisha mifupa ya uti wa mgongo,ingawa hakuna utafiti wa kutosha kuthibitisha kwamba mojawapo ni bora kuliko taratibu nyingine.[55] Kuongeza kipandikizi cha uti wakati wa kuunganisha mifupa hiyo huongeza hatari lakini hakuna manufaa zaidi dhidi ya maumivu au utendakazi wa mwili.[30]
Matibabu mbadalaSi wazi ikiwa utunzaji watibamwili au tiba yaunyooshaji wa uti wa mgongo hupelekea matokeo bora zaidi au chini ya matibabu mengine katika watu wenye maumivu ya mgongo.[56] Baadhi ya utafiti umegundua kuwa unyooshaji wa uti wa mgongo hupelekea matokeo sawia au hata bora dhidi ya maumivu na kuwezesha utendakazi, ikilinganishwa na matibabu ya kawaida yanayotumika kwa muda mfupi, muda wa kadri au wa kudumu.[57][58] Watafiti wengine walitambua kuwa unyooshaji wa uti wa mgongo si bora katika kupunguza maumivu kuliko matibabu mengine ya kutumia dawa, unyooshaji duni wa maungo, au matibabu mengine. Watafiti hawa walipendekeza kuwa kujumuisha mbinu ya unyooshaji wa uti wa mgongo katika matibabu mengine hupelekea matokeo bora.[59][5] Miongozo ya kitaifa imefikia maoni mbalimbali, huku baadhi yao wakikataa kupendekeza unyooshaji wa uti wa mgongo, wengine wakieleza kuwa unyooshaji hutegemea chaguo la mtu, huku wengine wakipendekeza unyooshaji kwa kipindi kifupi katika watu wasioimarishwa na matibabu mengine.[18] Unyooshaji wa uti wa mgongo chini ya anestesia, au unyooshaji kwa usaidizi wa dawa, hauna utafiti wa kutosha ili kuupendekeza kwa ujasiri.[60]
Tibapini ni sawa tu na kipoza ungo, utunzaji wa kawaida au bandia unaohusu tibapini dhidi ya maumivu ya ghafla yasiyo na asili bayana au maumivu sugu kidogo.[61] Katika watu wenye maumivu sugu, matibabu haya hupunguza maumivu kwa kiwango kidogo kuliko pasipo na matibabu yoyote, na huwa na matokeo sawa na ya kutumia dawa, lakini hayasaidii katika ulemavu.[61] Manufaa ya dawa hii kwa maumivu hudhihirika baada ya matibabu tu, wala si baadaye katika ufuatilizi.[61] Tibapini inaweza kuwa hatua bora katika watu wenye maumivu sugu yasiyotatuliwa kwa matibabu mengine kama vile dawa au matibabu yoyote yasiyohusisha upasuaji.[1][62] Ingawamatibabu ya upapasaji hayaonekani kupelekea manufaa mengi katika watu wenye maumivu ya ghafla, [1]upapasaji unaweza kusaidia watu wenye maumivu sugu kidogo, na pia maumivu sugu; hususan ukifanywa pamoja na mazoezi ya mwili na elimu ya afya.[63] Utafiti mmoja maarufu umependekeza kuwa tibapini na upapasaji kwa pamoja ni bora kuliko upapasaji pekee.[63]Prolotherafi –kudungia viowevu kwenye viunga vya mgongo ili kusababisha inflamesheni, hivyo kuchochea utaratibu wa mwili wa uponyaji – ni mbinu ambayo haijawahi kufaulu ikitumika pekee, lakini inaweza kusaidia inapojumuisha tiba nyingine.[5] Nurofleksotherapi, ni matibabu ambapo kipande cha chuma huingizwa chini ya ngozi ya sikio na mgongo. Matibabu haya yamegunduliwa kuwa bora katika kupunguza maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo na pia kuimarisha utendakazi wa mgongo wenyewe. Hata hivyo, tafiti zinazopendekeza mbinu hii ni chache.[5][64] Matibabu ya mitishamba kamammea unaobana nawillow nyeupeyanaweza kupunguza idadi ya watu wanaoripoti kiwango kikubwa cha maumivu; ingawa katika watu wanotumia dawa za kutuliza maumivu, tofauti yake si kubwa.[5] Kapsikamu – ya muundo wa mafuta au plasta – imetambulika kutuliza maumivu na kuimarisha utendakazi wa mgongo.[5]
[Matibabu ya kitabia]] yanaweza kusaidia watu wenye maumivu sugu.[65] Kuna aina mbalimbali za matibabu haya, ikiwa ni pamoja na uratibishaji tabia, ambayo ni njia ambapo kiimarishi hutumika kupunguza tabia mbaya na kukuza tabia njema; matibabu ya utambuzi wa tabia,ambayo husaidia watu kutambua na kubadilisha mawazo mabaya na tabia; na uratibishaji wa mwitikio, ni hatua zinazoweza kubadilisha mwitikio wa maumivu kisaikolojia kwa mtu binafsi. Wahudumu wa afya wanaweza kuunda mradi unganifu wa matibabu ya kitabia.[5] Utafiti haujaweza kubainii iwapo Upunguzaji wa mfadhaiko kupitia uzingatifu utapunguza ukali wa maumivu ya mgongo au ulemavu unaohusiana na maumivu ya mgongo. Hata hivyo, utafiti huu unaashiria kuwa hatua hii inaweza kumwezesha mtu kukabiliana na maumivu yaliyopo.[66]
MatarajioKwa kijumla, matokeo ya matibabu ya maumivu ya ghafla ya kiuno huwa mema. Maumivu na ulemavu hutatulika pakubwa katika wiki sita za kwanza, huku asilimia 40 – 90 ya watu wakipona kabisa.[67] Katika watu watakaokuwa na dalili za hali hii baada ya wiki sita, kuimarika kwao huwa taratibu, huku mabadiliko machache yakifikiwa kwa mwaka mmoja. Kufikia mwaka mmoja, kiwango cha maumivu na ulemavu huwa cha chini katika watu wengi. Kwa bahati mbaya, maumivu ya awali ya mgongo na kuridhika kazini hutumika kutabiri matokeo ya maumivu ya mgongo baada ya tukio la ghafla la maumivu.[67] Matatizo mengine ya kisaikolojia kama vile mfadhaiko au kukosa furaha kufuatia kupoteza kazi kunaweza kuzidisha maumivu ya mgongo kwa muda mrefu.[4] Kurejea kwa maumivu baada ya kisa cha kwanza hutokea katika zaidi ya nusu ya waathiriwa.[2]
Katika watu wenye maumivu sugu, matokeo ya kipindi kifupi huwa mema, huku kukiwa na mafanikio katika wiki sita za kwanza, lakini kuna mafanikio madogo baadaye. Kufikia mwaka mmoja, watu wenye maumivu sugu huendelea kupata maumivu ya kadri na ulemavu.[67] Watu walio katika hatari ya kupata ulemavu wa kudumu kwa kipindi kirefu ni pamoja na watu wasio na uwezo wa kukabiliana na maumivu au wanaoogopa kujishugulisha (wana uwezekano wa kupata matokeo mabaya mara 2.5 zaidi kwa mwaka), [68] watu wenye uwezo duni wa kukabiliana na maumivu, ulemavu wa kiutendaji, udhaifu wa afya ya kijumla, au kisababishi kikuu cha kiakili au cha kisaikolojia cha maumivu (Dalili za Waddell).[68]
EpidemiolojiaMaumivu ya sehemu ya chini ya mgongo yanayohudumu kwa siku moja na kulemaza kazi ya mtu ni hali inayoripotiwa mara nyingi.[31]Duniani, takriban 40% ya watu hupata maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo wakati mmoja maishani,[31] huku makadirio yakiwa hata 80% katika watu wa nchi zilizostawi.[69] Takriban asilimia 9 hadi 12 ya watu (milioni 632) hupata maumivu ya mgongo wakati wowote maishani, na karibu robo moja (23.2%) huripoti kuwa wamepata maumivu haya kwa wakati fulani katika kipindi cha mwezi wowote mmoja.[31][70] Matatizo mara nyingi hutokea kati ya umri wa miaka 20 na 40.[1] Visa vya maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo ni vingi katika watu wa umri wa miaka 40-80, huku wastani wa idadi ya watu wanaoathirika ikitarajiwa kuongezeka jinsi watu wanavyoendelea kuzeeka.[31]Haijulikani wazi iwapo ni wanaume au wanawake wanaoripoti visa vingi vya maumivu ya mgongo.[31][70] Utafiti wa mwaka wa 2012 uliripoti kima cha 9.6% miongoni mwa wanaume na 8.7% miongoni mwa wanawake.[70] Utafiti mwingine wa mwaka 2012 ulipata kima cha juu kwa wanawake kuliko wanaume. Watafiti walikisia kuwa takwimu hizi huenda zilichangiwa na maumivu kutokana na osteoporosisi, hedhi, na ujauzito miongoni mwa wanawake, au kwa sababu wanawake walikuwa tayari Zaidi kuripoti maumivu kuliko wanaume.[31] Takriban 70% ya wanawake hupata maumivu ya mgongo katika ujauzito, huku kima cha maumivu kikiongezeka ujauzito unapokomaa.[71] Wavuta sigara katika ujauzito – hususan wanawake wa umri wa kubaleghe – wana uwezekano mkubwa wa kupata maumivu ya mgongo kuliko waliokuwa wakivuta awali, na wanawake waliokuwa wakivuta sigara awali wana uwezekano mkubwa kuliko wale ambao hawajawahi kuvuta.[72]
Historia
Harvey Williams Cushing, 1920sMaumivu ya kiuno yamewaathiri watu tangu enzi za shaba. Makala ya upasuaji wa kale yanayojulikana kama Mafunjo ya Edwin Smith katika enzi ya 1500 KK yalieleza kuhusu uchunguzi tambuzi na matibabu ya mkazo wa pingili za uti wa mgongo.
Hippocrates (460 KK hivi – 370 KK hivi) alikuwa wa kwanza kutumia neno kurejelea maumivu ya nyonga na ya kiuno; Galen (enzi za kati hadi mwishoni mwa karne ya 2 BK) alielezea suala hili kwa kina. Madaktari mwishoni mwa milenia ya 1 hawakujaribu upasuaji wa mgongo. Baadala yake, walipendekeza kusubiri kwa umakinifu.
Katika enzi za kati, waganga wa kale walitoa matibabu ya maumivu ya mgongo wakiamini kuwa yalisababishwa na mapepo.[73]
Mwanzoni mwa karne ya 20, madaktari waliamini kuwa maumivu ya mgongo yalisababishwa na inflamesheni au kuharibika kwa neva,[73] huku hali ya niuraljia na niuraitisi ikitajika mara nyingi katika fasihi za wakati huo.[74] Hata hivyo, katika karne ya 20, imani ya visababishi hivi ilididimia.[74]
Mwanzoni mwa karne wa 20, mpasuaji wa mfumoneva wa Marekani Harvey Williams Cushing aliongeza umaarufu wa matibabu ya maumivu ya mgongo kupitia upasuaji.[53] Katika miaka ya 1920 na 1930, nadharia geni zilizuka, huku madaktari wakidokeza kuna uhusiano kati ya mfumo wa neva na matatizo ya kisaikolojia kama vile ulegevu wa neva (niurasthenia) na histeria ya wanawake.[73] Rimathoidi ya misuli (fibromiljia) pia ilitajwa sana.[74]
Vifaa vya kisasa vya teknolojia, kama vile Eksirei viliwapa madaktari vifaa vipya vya utambuzi, hivyo kufichua kuwa diski ya kati ya pingili za uti wa mgongo ndizo zilizokuwa chanzo cha maumivu ya mgongo katika baadhi ya visa. Mwaka wa 1938 mpasuaji wa mifupa, Joseph S. Barr, aliripoti kuwa maumivu ya nyonga yanayohusiana na diski yaliimarika au kuponywa kupitia upasuaji wa mgongo.[74] Kufuatia ripoti hii, umbo la mfano wa diski lilitolewa miaka ya 1940,[73] na kuvuma katika fasihi katika miaka ya 1980 na kusaidia kuzinduliwa kwa pichatiba nyingine kama vile Tomografia ya Kompyuta na Picha za Mwangwi wa Sumaku.[74]
Mjadala huu ulififia utafiti ulipoonyesha kuwa matatizo ya diski si kisababishi kikuu cha maumivu. Tangu wakati huo, madaktari waligundua kuwa mara nyingi kuna uwezekano ya kisababishi maalumu cha maumivu ya mgongo kutobainika, hivyo wakakosoa haja ya kupata angalau kisababishi kimoja kwa sababu wakati mwingi dalili hizi zilipotea katika wiki 6 hadi 12 matibabu yasipokuwepo au yakiwepo.[73]
Jamii na utamaduniMaumivu ya sehemu ya chini ya mgongo husababisha gharama ya kiuchumi ya kiwango cha juu. Nchini Marekani, maumivu ya mgongo ni aina kuu ya maumivu katika watu wazima yanayosababisha idadi kubwa ya watu kutokwenda kazini. Halii hii pia ni tatizo kuu la misuli na mifupa linaloripotiwa mara nyingi katika kitengo cha matibabu ya dharura.[6]Mwaka wa 1998, ilikadiriwa kuwa gharama ya maumivu haya ni bilioni $90 katika bajeti ya afya ya kila mwaka, huku 5% ya watu wakigharamia kiasi kikubwa zaidi (75%).[6] Kati ya 1990 na 2001, kulikuwa na ongezeko la zaidi ya mikunjo miwili ya uunganishaji wa mifupa ya uti wa mgongo nchini Marekani, hata ingawa hakukuwa na mabadiliko ya viashirio vya upasuaji au utafiti kuhusu umuhimu wa upasuaji.[30] Gharama zaidi huingia kupitia kufifia kwa utendakazi wa mtu na kupata mapato ya chini, huku maumivu ya mgongo yakichangia 40% ya siku zote ambazo watu walikosa kufika kazini nchini Marekani.[75] Maumivu ya mgongo husababisha ulemavu kwa asilimia kubwa ya wafanyakazi nchini Kanada, Uingereza, Uholanzi na Uswisi kuliko Marekani au Ujerumani.[75]
UtafitiUbadilishaji wa diski nzima ni chaguo la kujaribia,[15] lakini hakuna ushahidi wa kutosha unaopendekeza manufaa ya ubadilishaji huu kuliko uunganishaji wa mifupa ya kiuno.[53] Watafiti wanachunguza uwezekano wa kukuza diski mpya wakitumia dawa ya ukuaji inayodungwa binadamu; vipandikizo, tibaseli, na uhandisi wa tishu.[15]