Ugonjwa Wa Bawasili, Madhara Yake, Sababu, Dalili, Matibabu Na Dawa Sahihi
Ugonjwa wa bawasili ni ugonjwa ambao waathirika wengi hupata aibu kuuzungumzia kutokana na mahala ugonjwa huo ulipo. Lakini kuna msemo usemao mfinya maradhi mauti humuumbua. Huu ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine, unahitaji kutibiwa kwa haraka kabla haujaleta madhara makubwa kiafya. Katika makala yetu haya tutazungumza kwa undani na mapana sana juu ya:
- Bawasili ni nini
- Aina za bawasili
- Sababu za bawasili
- Dalili za bawasili
- Madhara ya bawasili
- Matibabu na dawa sahihi
- NINI KINASABABISHA BAWASILI?
- Miongoni mwa visababishi vya bawasir ni;
- Tatizo sugu la kuharisha
- Kupata haja kubwa(kinyesi)kigumu
- Uzito kupita kiasi (OBERSITY)
- Ngono ya njia ya haja kubwa (ANAL SEX)
- Umri mkubwa na mambo yanayoongeza shinikizo katika tumbo.
- Kukaa muda mrefu
DALILI ZA BAWASIRI- Kinyesi kuchanganyika na damu wakati wa kujisaidia
- Maumivu au usumbufu katika njia ya haja kubwa
- Kutokwa na kinyesi bila kujitambua(kuvuja kinyesi)
- Kijiuvimbe katika eneo la tundu(mlango)wa kutolea haja kubwa.
- Ngozi katika eneo la tundu la haja kubwa kuwasha.
- Bawasiri kutoka wakati wa kujisaidia haja kubwa.
ATHARI ZA BAWASIRI
Upungufu wa damu mwilini (ANEMIA) - STRAGULATED HEMORRHOID
- Kinyesi kutoka na kuvuja bila kujitambua na kusababisha kunuka kinyesi saa zote.
- Kukupunguzia morali ya kufanya kazi kutokana na maumivu hasa watu wanaokaa muda mrefu maofisini.
- Kuathirika kisaikolojia
- Kukosa hamu ya tendo la ndoa.
- Kupungukiwa nguvu za kiume.